The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MAGARI SABA YAKABIDHIWA KWA KANDA NA VYUO VYA VETA KUBORESHA SHUGHULI ZA UTOAJI WA MAFUNZO
Posted on: Tuesday, 21 March 2023
MAGARI SABA YAKABIDHIWA KWA KANDA NA VYUO VYA VETA KUBORESHA SHUGHULI ZA UTOAJI WA MAFUNZO YA UFUNDI STADI
Tarehe 20 Machi, 2023, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amekabidhi magari saba kwa Kanda na vyuo vya VETA ili kuboresha utekelezaji wa shughuli za utoaji elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Magari hayo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.19 yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini na Wakuu wa vyuo vya VETA vya Kanadi, Ndolage, Ruangwa, Nyasa, Newala na Ngorongoro.
CPA. Kasore amesema kasi ya ukuaji wa Mamlaka hiyo inayotokana na ujenzi wa vyuo vipya na kupanuka kwa shughuli za mafunzo kumepelekea ongezeko la uhitaji wa magari na kwamba jitihada mbalimbali zimeendelea kufanyika ili kukidhi mahitaji hayo.
“Jitihada zinazofanywa na Mamlaka ni pamoja na kutenga bajeti kila mwaka wa fedha kwa ajili ya kununua magari mapya pamoja na kuomba magari kwa wadau mbalimbali,”amesema
Aidha, CPA Kasore ameagiza Wakuu hao kuzingatia na kusimamia matumizi sahihi ya magari hayo na kuhakikisha yanatunzwa na kufanyiwa matengenezo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa VETA,Ndugu Felix Staki, amesema ugawaji wa magari hayo katika awamu hii umezingatia umbali wa vyuo na maeneo ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kwamba vyuo vingine vitaendelea kupatiwa magari hayo kadri yatakavyoendelea kupatikana.