The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA yaihakikishia jamii utayari wake utekelezaji wa mabadiliko ya mitaala ya Sekondari
Posted on: Tuesday, 05 December 2023
VETA yaihakikishia jamii utayari wake utekelezaji wa mabadiliko ya mitaala ya Sekondari
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeihakikishia jamii utayari wake katika utekelezaji wa mitaala mipya ya Sekondari kwa upande wa utoaji mafunzo ya amali.
Meneja Uhusiano wa VETA, Ndg. Sitta Peter, amesema hayo tarehe 3 Desemba, 2023, wakati wa kuhitimisha maonesho ya miaka 50 ya NECTA yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini, Dar es salaam.
Ametaja baadhi ya majukumu ya VETA kwenye utekelezaji wa mitaala hiyo kuwa ni kuandaa mitaala na vitabu vya kufundishia mafunzo ya amali na kusimamia utoaji wa mafunzo hayo kwa ufanisi.
Amesema, tayari VETA imeshaandaa mitaala, miongozo na vitini kwa ajili ya mafunzo ya amali shule za sekondari, ambayo yanatarajiwa kuanza Januari, 2024.
Sambamba na hilo ametoa wito kwa wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne kujipatia ujuzi katika vyuo vya VETA nchini katika kipindi cha mpito wanachosubiria kuendelea na hatua zingine za masomo.
Amesema ujuzi huo utakuwa akiba kwenye maisha yao na kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa.