The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mia moja waomba kujiunga na chuo kipya cha VETA Ulanga
Posted on: Monday, 19 February 2024
Mia moja waomba kujiunga na chuo kipya cha VETA Ulanga
Vijana 100 kutoka wilaya ya Ulanga na maeneo ya jirani wameomba kujiunga na fani za muda mrefu katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ulanga (VETA Ulanga) kwa mwaka wa masomo wa 2024.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Msajili wa Chuo hicho, Mhandisi Benitho Kigava mafunzo katika chuo hicho yataanza na fani za Umeme wa Majumbani (EL); Ushonaji, Ubunifu wa Mavazi na Teknolojia ya Nguo (DSCT); Uashi na Ufundi Bomba.
Kigava amesema usaili wa vijana walioomba ulifanyika tarehe 13 Februari 2024 katika maeneo mbalimbali ikiwemo, kituo cha Mwaya, Ulanga (Chuo cha VETA) ambako vijana 54 wamejitokeza; kituo cha Mahenge mjini vijana 23; kituo cha Ifakara, vijana 14 na kituo cha Mikumi, vijana 9.
“Tunaamini baada ya selection (uchaguzi) tutapata vijana 80 kukidhi idadi ya wanafunzi 20 kwa kila fani,” amesema.
Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ulanga ni miongoni mwa vyuo 29 vipya vya VETA ambavyo vinaanza kutoka mafunzo ya ufundi stadi mwaka huu, 2024.