The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
WAFANYAKAZI VETA KANDA YA KASKAZINI WANOLEWA MATUMIZI YA GAMIS
Posted on: Friday, 21 April 2023
WAFANYAKAZI VETA KANDA YA KASKAZINI WANOLEWA MATUMIZI YA GAMIS
Jumla ya wafanyakazi 50 wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Kaskazini wamepatiwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMIS) kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kusimamia mali za Umma.
Mafunzo hayo yalifanyika katika chuo cha VETA Tanga, tarehe 17 hadi 19, Aprili 2023 chini ya uwezeshaji wa Kaimu Meneja Miliki wa VETA, Bi. Furaha Paul.
Akizungumzakuhusuumuhimuwa mafunzo hayo, Kaimu Meneja Miliki wa VETA, Bi Furaha Paul, alisema mfumo huo utawezesha upatikanaji wa sahihi na kwa wakati taarifa za mali zinazohusu hali, thamani, uchakataji wa uchakavu (depreciation), idadi na mahali zilipo, hivyo kuwezesha Serikali kufanya maamuzi sahihi kuhusu mali zake.
“Mfumo huu utasaidia kuongeza udhibiti wa mali, kuwezesha kufanya uchambuzi wa taarifa na kuzichakata na hatimaye kutoa taarifa mbalimbali za mali,” alisema
Kwa mujibu wa Bi. Furaha, mfumo huo utawezesha kuongeza uwazi na uwajibika katika usimamizi wa mali za Serikali na kuleta ufanisi katika ukusanyaji na udhibiti wa mapato yanayotokana na mauzo ya mali chakavu, malipo ya tozo mbalimbali zinazotokana na upotevu au ajali ya mali za Serikali.
Aliwasisitiza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kujenga utamaduni wa ukutunza mali ikiwa ni pamoja kuweka taarifa za mali ambazo ni sahihi kwenye mfumo ili kupunguza changamoto zilizojitokeza katika daftari la mali la Mamlaka kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo huo.
Naye Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini, Bi. Monica Mbele, aliwaagiza wafayakazi hao kufuata maelekezo yaliyotolea hasa katika matumizi ya mfumo huo na kuwasisitiza kuzingatia taratibu sahihi wakati wa uingizaji wa taarifa hizo.
Pamoja na mafunzo yaliyotolewa, wafanyakazi hao walipata fursa ya kupitia taarifa za mali zilizoko katika Kanda ya Kaskazini.