The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Wajumbe wa Bodi ya VETA Board watembelea kiwanda cha samani VETA Dodoma
Posted on: Friday, 22 December 2023
Wajumbe wa Bodi ya Tisa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Sifuni Mchome, tarehe 21 Desemba, 2023 wametembelea kiwanda cha kutengeneza Samani cha VETA jijini Dodoma kujionea shughuli za uzalishaji samani zinavyoendeshwa kiwandani hapo.
Kabla ya ziara hiyo, wajumbe hao walikutana katika kikao maalum cha Bodi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano VETA Makao Makuu jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali inayolenga kuimarisha utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.