The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mkurugenzi Mkuu amekagua Kikao Kazi cha uhariri wa vitini kwa ajili ya mafunzo ya amali
Posted on: Thursday, 16 November 2023
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Prosper Mgaya, tarehe 15 November 2023 amekagua Kikao Kazi cha uhariri wa vitini kwa ajili ya mafunzo ya amali kwenye shule za sekondari nchini, kinachofanyika katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Kampasi ya Morogoro (WAMO). Uandaaji wa vitini hivyo unafanywa na wataaamu wa fani mbalimbali chini ya usimamizi wa VETA kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Amewapongeza wataalamu kwa kujitoa kwao kwa juhudi na maarifa kufanya kazi hiyo. Amewasihi kutunza vyema kumbukumbu za kazi iliyofanyika na kujiandaa kwa utungaji wa vitabu baada ya kazi ya vitini kukamilika.